• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mkurugenzi Ilemela aelekeze ujenzi wa miundombinu Shule ya Sekondari Igogwe kuanza mara moja

Posted on: April 14th, 2022

Mhandisi Modest Apolinary, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela ameutaka uongozi wa Kata ya Bugogwa kuhakikisha ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari ya Igogwe unaanza mara moja huku akisisitiza kuhusu suala la mafundi na vibarua watakaohusika na ujenzi huo kutoka ndani ya kata ya Bugogwa.


“Tungependa mafundi na vibarua watoke hapa tusije kukuta fundi au vibarua wanatoka mjini wote watoke katika mazingira haya ili hizi fedha zote zibaki kwenye kata hii  ni imani yangu baada ya kukamilika kwa ujenzi huu vijana wetu watakuwa wameshapata mitaji ya kuendelea na biashara zao kwasababu hizi fedha tungependa zibaki hapahapa”, Amesema Mhandisi Apolinary


Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa program ya mpango wa kupunguza umaskini (TPRP- IV) kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF)  katika Manispaa ya Ilemela.

Aidha alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa Afisa elimu Sekondari kuhakikisha kuwa vyoo katika shule hiyo vinakamilika ndani ya wiki mbili ili watoto waanze kutumia miundominu ya madarasa manne  yaliyopo katika shule ya sekondari ya Igogwe yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi wa kata ya Bugogwa huku ujenzi wa miundombinu mingine ukiendelea


Nae mratibu wa TASAF- Ilemela Ndugu Frank Ngitao alibainisha kuwa Ilemela imeshapokea kiasi cha shilingi Milion 308.56 ikiwa ni awamu ya kwanza kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi iliyoombewa fedha ambapo alisema kuwa fedha hiyo itatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule ya sekondari Bugogwa ambapo itatekelezwa na mitaa mitano ya Kata ya Bugogwa.


Aliongeza kusema kuwa utekelezaji wa miradi hii utafanywa na jamii kupitia kamati za usimamizi wa shughuli za TASAF katika mitaa husika chini ya usimamizi wa wataalam wa Ilemela na sekta husika kwa kuzingatia miongozo ya TASAF huku akisema kuwa miradi hii inatakiwa kukamilishwa  katika kipindi cha miezi mitatu, kuanzia mwezi Aprili hadi Julai 2022.


Nae Diwani wa Kata ya Bugogwa Mhe. William Mashamba pamoja na kuishukuru serikali kwa mradi huu amewataka wananchi wa kata hiyo Kila mmoja kuwa  askari wa mwenzake huu kwani huu ni mradi ni wao, huku akiwahimiza vijana kufanya kazi kwa bidi kwani kupitia mradi huu wamepata ajira.


Wananchi wa Kata Bugogwa hususana mitaa ya Nkoloto, Masemele B, Igogwe A, Bugolanya na Isanzu ambao watatekeleza awamu ya kwanza ya mradi wameishukuru serikali kwa kuwajali huku wakiomba changamoto za nyumba za walimu kutatuliwa ili walimu waweze kuishi maeneo jirani na shule.


Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ni kati ya Halmashauri 33 nchini zinazotekeleza mradi  wa kupunguza umaskini awamu ya nne kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)  ambao utajumuisha miradi ya ujenzi wa miundombinu ya afya , elimu na maji, miradi ya ajira za muda pamoja na miradi ya kukuza kipato cha kaya.











Announcements

  • TANGAZO LA KAZI NAFASI YA UDEREVA DARAJA LA II June 04, 2025
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • ELIMU YA FEDHA KUWAONGEZEA UFANISI WANUFAIKA WA TASAF

    July 03, 2025
  • AWAMU YA KWANZA UCHANJAJI MIFUGO KUANZA TAREHE 03 JULAI, KUKU ELFU 70 KUCHANJWA

    July 02, 2025
  • KAMPENI YA KITAIFA YA UTOAJI WA MATONE YA VITAMI A YAFIKIA ASILIMIA 98.7

    June 26, 2025
  • WENZA WA VIONGOZI WATEMBELEA SEKONDARI YA IGOGWE WAPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI

    June 26, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.