Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mhe. Dkt Angeline Mabula amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Nyanza Road Works anaejenga barabara ya Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongolo kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa na wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano
Mhe Mabula ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Jimbo hilo pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Nyamhongolo.
'.. Nimeridhishwa na hatua za ujenzi wa mradi isipokuwa nimuombe mkandarasi kuongeza kasi yake ya ujenzi pamoja na kuzingatia ushauri tunaoutoa ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazolalamikiwa na wananchi katika mradi huu kama uwekaji wa njia za mchepuko ..' Alisema
Kwa upande wake mratibu wa miradi ya kimkakati na uendelezaji wa majiji TACTIC wilaya ya Ilemela Mhandisi Juma King'ola amefafanua kuwa mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 28.72 na kwamba mradi wote utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 23.49 na unatarajiwa kukamilika mnamo februari 2025 na mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi bilioni 3.5
Juma Maro ni Mhandisi mkadiriaji majenzi ambae pia ni mwakilishi wa mkandarasi anaetekeleza mradi huo kampuni ya ujenzi Nyanza ambapo amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo ulikabiliwa na changamoto za mvua, uchelewaji wa uhamishaji wa miundombinu ya maji na umeme pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara ya baadhi ya michoro kulingana na uhitaji wa wakati huku akiahidi kukamilisha kwa wakati mradi huo
Nae diwani wa kata ya Nyamhongolo Mhe Andrea Nginila mbali na kuishukuru Serikali kwa mradi huo amelalamikia vumbi wakati wa ujenzi wa mradi linalosumbua wananchi wake pamoja na kutokuwepo kwa njia za mchepuko za kutosha hivyo kuomba kuongezwa
Mradi wa ujenzi wa barabara za Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongolo na Buswelu-Busenga-Cocacola zenye urefu wa kilomita 12.8 ulianza kutekelezwa mapema mnamo Novemba 19, 2024 kwa ufadhili wa benki ya dunia kupitia mpango wake wa uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania (TACTIC)
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.