MIRADI SABA (7) YENYE THAMANI YA SHILINGI ZA KITANZANIA 2,094,893,888.90 YATEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU 2017
Wilaya ya Ilemela iliupokea Mwenge wa Uhuru mnamo tarehe 21/08/2016 katika kata ya Nyakato eneo la uwanja wa Kingunge ukitokea Wilaya ya Nyamagana na kuukimbiza kwa siku moja umbali wa kilometa 51.9 na kisha kuukabidhi Wilaya ya Ukerewe siku ya tarehe 22/08/2017.
Ukiwa Wilayani Ilemela, Mwenge wa Uhuru 2017, ulifungua, ulizindua, ulikagua na kuweka jiwe la msingi. Jumla ya miradi iliyopitiwa na Mwenge ni saba(7) yenye thamani ya shilingi za kitanzania 2,094,893,888.90, thamani ya miradi hii imetokana na michango ya serikali kuu Tshs. 1,306,758,024.90, Wananchi Tshs. 33,341,243.00, Halmashauri Tshs. 84,400,000.00 na wahisani Tshs. 670,394,621.
Mwenge wa Uhuru 2017, uliweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya buswelu.Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh.91,569,710.20 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu halmashauri,nguvu za wananchi na wahisani.Pia katika shule hiyo uliweza kukagua klabu ya wapinga rushwa.
Mradi mwingine uliotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2017 ni ujenzi wa tanki la maji nyamadoke ambapo uliweka jiwe la msingi.Mradi huu hadi hatua ilipofikia umegharimu kiasi cha Tsh.1,156,603,085.70 ikiwa ni fedha kutoka serikali Kuu,halmashauri na nguvu za wananchi.wakiwa katika mradi huu wamehimiza kuwa mradi ukamilishwe ili kuweza kutatua changamoto ya maji katika eneo hilo.
Ukiwa Wilayani Ilemela Mwenge wa Uhuru ulikagua shamba la mkulima wa mfano lililopo kata ya shibula lililoanzishwa kwa madhumuni ya kujipatia kipato pamoja na kuhifadhi mazingira.Mradi huu ambao ulianza mwaka 2012 kwa sasa umeanza kutumika kama mfano kwa wakulima wengine wa ndani na nje ya Manispaa ya ilemela.
Katika kata ya shibula Mwenge ulifanya ufunguzi wa zahanati ya Buganda ambayo hadi kukamilika imegharimu kiasi cha Tshs. 133,776,472.00 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu halmashauri na nguvu za wananchi.Ukiwa katika zahanati hiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru alitoa vyandarua na dawa za malaria kwa wamama wajawazito ikiwa ni harakati za kupambana na malaria.Pamoja na hayo mkimbiza mwenge aliwataka wahudumu wa zahanati hiyo kutoa huduma bora na kwa usawa na kuwataka wananchi kuitunza zahanati hiyo.
Katika kata ya Pasiansi, Mwenge wa Uhuru ulizindua ofisi ya mtendaji wa kata hiyo.mradi huo umegharimu kiasi cha Tshs.44,800,000.00 ikiwa ni fedha za halmashauri pamoja na nguvu za wananchi.Aidha kiongozi wa mbio za mwenge aliwataka watumishi wa kata hiyo kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia taratibu za kazi pamoja na hayo aligusia suala la utatuzi wa migogoro kuwa lianzie ngazi ya kata.
Mwenge wa Uhuru ulifanya ukaguzi katika kituo cha kusaidia waathirika wa dawa za kulevya katika kituo cha pili Missanah foundation.Katika kituo hicho alishauri halmashauri kuendelea kushirikiana na kituo hicho aidha alikabidhi msaada wa chakula kwa kituo hicho kilichonunuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa.
Mradi wa mwisho ulikuwa wa ujenzi wa barabara ya mawe ya kawekamo, mradi huu uliogharimu kiasi cha Tshs.464,244,621.00 fedha ya wahisani ulizinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge na kisha kuwataka wananchi kufuata sheria za usalama barabarani.
Mwenge wa Uhuru 2017 umekimbizwa wilayani Ilemela ukieneza Kauli mbiu isemayo "Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu".
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.