Mikataba mitano (5) yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.49 imesainiwa leo na Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mhandisi Modest Joseph Apolinary, Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela amesema kuwa asilimia kubwa ya fedha inayotekeleza miradi hiyo ni fedha za mapato ya ndani ambayo ni takribani Bilioni 1.45 kwa miradi ya barabara sambamba na uchimbaji wa kisima na kiasi cha shilingi milioni 40.4 ni fedha kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka.
Mikataba hiyo iliyosainiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kuelekea hospitali mpya ya Wilaya yenye urefu wa km 1.5,ujenzi wa barabara kuingilia stendi ya daladala Nyamhongolo, barabara ya Igombe ziwani yenye urefu wa km 0.14,ujenzi wa kisima cha maji safi eneo la ofisi za makao makuu na ujenzi wa kichomea taka katika hospitali mpya ya Wilaya.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mhe. Renatus Mulunga Akizungumza wakati hafla fupi ya kusaini mikataba hiyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwa wamoja ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi
“Nimshukuru Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazozitoa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa yake pamoja na niwatake watumishi wa umma kuzisimamia na kuilinda ili tija inayotakiwa iweze kupatikana”, Amesema Mhe Mulunga
Kwa niaba ya wazabuni walioshinda zabuni hizo Bwana James Cyprian Siingwa ambae ni mwakilishi wa kampuni ya Engineering and Business Suport Investment Ltd iliyopata kazi ya kutekeleza mradi wa kichomea taka ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo na kuwahakikishia wananchi kuwa kazi waliyopewa wataikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
PICHA ZA MATUKIO YA KUSAINI MIKATABA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.