Mashindano ya michezo kwa shule za sekondari maarufu kwa jina la umiseta yametakiwa kutumika kama sehemu ya kuchochea ukuaji wa taaluma na nidhamu kwa wanafunzi wanapokuwepo mashuleni
Rai hiyo imetolewa na afisa elimu sekondari wa manispaa ya ilemela mwalimu sylvester mrimi wakati wa shughuli ya kufunga mashindano ya umiseta kiwilaya iliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya wavulana bwiru ambapo amewaasa walimu na wanafunzi kutumia fursa ya uwepo wa mashindano hayo kama sehemu ya kuonyesha vipaji na kukuza taaluma
'.. Ni matumaini yangu kuwa baada ya kuisha michezo hii hatutegemei kuona anayeshiriki michezo ndio anaefeli, tunategemea kuona heshima, maadili, uvumilivu, adabu, na bidii ..' alisema
Aidha mwalimu mrimi mbali na kumshukuru rais mhe dkt samia suluhu hasan kwa fedha anazozitoa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule ameihakikishia timu ya wilaya ya ilemela ushirikiano katika kushiriki kwake ngazi ya mkoa sanjari na kuitaka ikafanye vizuri na kurudi na vikombe vya ushindi
Nae afisa elimu vifaa na takwimu sekondari wa manispaa ya ilemela mwalimu hellen mushi amefafanua kuwa michezo ya umiseta kwa manispaa ya ilemela ilianza mei 31 na kuhitimishwa june 02, ikifadhiliwa na mkurugenzi wa manispaa hiyo pamoja na benki ya crdb ambapo shule 56 za binafsi na umma zimeshiriki huku michezo ya mpira wa meza na goli kwa walemavu ikiongezwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo haikuwepo kabisa
Kwa upande wake afisa michezo wa manispaa ya ilemela ambae pia ndie meneja wa timu ya wilaya mwalimu bahati kizito ametoa wito kwa wadau wa michezo na wasimamizi wa vilabu mbalimbali kutembelea viwanja yanapoendeshwa mashindano hayo kujionea vipaji na kuvisajili huku akitolea mfano wa mchezaji kelvin john anaechezea klabu ya nje ya nchi aliyeibuliwa kupitia mashindano hayo miaka kadha nyuma
Swaum daud ni mwanafunzi wa kidato cha pili kutoka shule ya sekondari pasiansi mbali na kushukuru kwa uwepo wa mashindano hayo yanayosaidia kukuza akili, ushirikiano, vipaji na afya ameahidi ushindi kwa ngazi ya mkoa pindi yatakapoanza
Mashindano ya UMISSETA kwa mwaka 2023 yamepambwa na kauli mbiu ya “uimarishaji wa miundombinu ya elimu nchini ni chachu ya maendeleo ya taaluma, sanaa na michezo” na kata ya pasiansi imefanikiwa kuibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo kwa ngazi ya wilaya ya ilemela kwa mwaka huu
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.