Katika kipindi cha miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika tija imeongezeka katika sekta mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali, na huduma za kijamii, utawala bora, ulinzi na usalama kwa ujumla katika kila sekta ndani ya Wilaya ya Ilemela
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana katika hotuba iliyosomwa na mwakilishi wake Ndugu Emili Kasagara katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya Uhuru
Kwa upande wa sekta ya viwanda amebainisha kuwa viwanda vingi vinamilikiwa na watanzania wenyewe na hivyo kutoa ajira kwa watanzania na kuongeza kuwa wakati wa utawala wa mkoloni Ilemela hapakuwa na viwanda vikubwa na vya kati ambapo hadi sasa vipo viwanda 12, vya kati 11 na vidogo 286.
Ndugu Kasagara ameongeza kusema kuwa hatua kubwa imepigwa katika sekta ya elimu ambapo hadi sasa zipo shule za msingi na awali 130 tofauti na awali ambapo zilikuwa shule 08 tu za serikali na kwa upande wa elimu sekondari wilaya ina shule 54 za sekondari ambapo shule 32 ni za serikali na shule 22 ni za watu binafsi, mashirika ya dini au taasisi.
Akizungumzia kuhusu suala la Maji Ndugu Kasagara amesema kuwa serikali inatambua changamoto ya maji kwa wananchi hususana Mkoa wa Mwanza na kusema kuwa juhudi zinaendelea kwa kujenga chanzo kikubwa cha maji cha Butimba kinachoenda kutatua tatizo kubwa la maji.
Kuhusu Sekta ya Afya amesema kuwa awali Wilaya haikuwa na kituo chochote cha kutolea hudu,a za afya, lakini kupitia jitihada serikali na wananchi jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vimejengwa ambapo zipo hospitali vinne, vituo vya afya 11 na zahanati 38, kliniki tisa na maternity home (vinne)
Ndugu Kasagara kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza amewasisitiza wananchi umuhimu wa kutumia fursa zilizopo za uwekezaji kuondoa umaskini wa kipato na kuboresha hali ya maisha ya wananchi wilaya ya Ilemela kiuchumi na kijamii.
Sherehe hizo za kilele cha maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru zilitoa fursa ya kongamano ambapo mada kubwa iliyojadiliwa ikiwa ni “ Maendeleo ya Tanzania baada ya Uhuru” ambapo mada mbalimbali juu ya elimu, afya, miundombinu, teknolojia na maendeleo ya kiuchumi ziliwasilishwa.
“Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo Yetu”, ni kauli ya mbiu ya miaka 61 ya Uhuru ambapo wananchi wametakiwa kuiishi kwa vitendo kwa kuhakikisha wanalinda na kudumisha Amani na Umoja kwani ndio tunu ya Taifa la Tanzania.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.