• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MHE. DKT. MPANGO AMEITAKA ILEMELAKUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO STENDI YA MABASI NYAMHONGOLO

Posted on: September 13th, 2022

Na Violencea Mbakile-Ilemela


Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuhakikisha inasimamia suala zima la ukusanyaji wa mapato katika stendi ya mabasi na eneo la maegesho ya malori Nyamhongolo kwa kuweka mifumo bora ya kielektroniki ya ukusanyaji mapato.

Mhe. Dkt Mpango ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa stendi hiyo mapema tarehe 13 septemba 2022 na kuitaka Ilemela kuwa mfano mzuri wa kuigwa wa ukusanyaji wa mapato katika stendi hii.


“Nataka Ilemela muwe ni mfano wa kuigwa wa kukusanya mapato katika kituo hiki , hakikisheni mnasimamia na kuweka mifumo bora ya kielektroniki ya ukusanyaji mapatio yanayotokana na kituo hiki, nisingependa kuona mapato yanapotea hivyo mianya yote ya upotevu wa mapato izibwe kabisa ”. Amesisitiza

Pamoja na hayo amehimiza kuwa anataka kuona mabadiliko katika suala zima la mapato ya Ilemela kufuatia ujenzi wa kituo hiki kwani kituo hiki ni fursa kubwa hivyo anatarajia kuona makusanyo yanaongezeka mara dufu na kuelekeza ufanyike usimamizi mzuri wa kituo.



Aidha amewataka wananchi kuchangamkia fursa za biashara na ajira zilizopo katika kituo hiki pamoja na kuhakikisha kuwa wanakitunza na kuendelea kuwa safi ili kiweze kudumu.


Nae Mbunge wa Ilemela  na Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe Dkt Angeline Mabula pamoja na kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ametumia fursa hiyo kuwasilisha kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Ilemela cha uhaba wa maji nakumuomba Makamu wa Rais kumsaidia kuiondoa kero hiyo ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Ilemela.


Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI awali akimkaribisha Makamu wa Rais, amemshukuru kwa kuridhia kufungua stendi hiyo na kumuahidi kutekeleza maagizo yote aliyotoa huku akimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kubainisha kuwa kupitia Serikali ya awamu ya sita Ilemela itanufaika na miradi wa kimkakati ambayo itahusisha ujenzi wa soko la Kirumba na barabara zinazonguka soko hilo, ujenzi wa Barabara za Buswelu-Busenga hadi CocaCola, na Ujenzi wa barabara ya Buswelu, Nyamadoke hadi Nyamhongolo ambapo miradi hii yote itagharimu kiasi cha fedha za kitanzania takriban Shilingi bilioni 28.8.


Mhe. Dkt Mpango, akihitimisha ametoa maagizo mbalimbali kwa uongozi wa Manispaa ya Ilemela, yakiwemo na kuhakikisha kuwa stendi inakuwa na majokofu ya kutunzia bidhaa zinazoharibika kwa kipindi kifupi, kuhakikisha ujenzi wa  jengo la machinga unaanza mara moja pamoja na kuhakikisha Manispaa ya Ilemela inaondoa kero ya vumbi na tope katika eneo la stendi ya daladala ikiwa ni pamoja na kupendezesha stendi kwa kupanda miti


Mradi wa Ujenzi wa stendi ya mabasi na eneo la maegesho ya malori Nyamhongolo hadi kukamilika kwake umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 26. 6 fedha za kitanzania ambao umejengwa na mkandarasi STECOL CORPORATION kampuni kutoka China, chini ya mtaalam mshauri (BICO) kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary.


Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.