• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI WA TAARIFA ZA FEDHA KUSAIDIA UDHIBITI WA FEDHA ZA UMMA

Posted on: June 13th, 2017

MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI WA TAARIFA ZA FEDHA  KUSAIDIA UDHIBITI WA FEDHA ZA UMMA



Mfumo wa Uhasibu na Utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma unaojulikana kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS) utasaidia udhibiti wa mapato na matumizi ya fedha za Umma sanjari na kuongeza Uwazi na Uwajibikaji  kwa vituo vya kutolea huduma za wananchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndugu Omary Kamatta alipokuwa akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji hilo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa katika vituo vya kutolea huduma yanayotolewa na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kama Public Sector System Strengthening (PS3) kwa wataalamu wa vituo vya afya na waratibu Elimu kutoka wilaya za Ilemela na Nyamagana kwa ufadhili wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ikishirikiana na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID)


“Zipo changamoto za upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali fedha zilizopo katika vituo vyetu vya huduma na hivyo halmashauri kushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya ruzuku zinazotolewa katika vituo hivyo wakati mwingine kusababisha halmashauri husika kupata hati ya mashaka kutoka kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG). Hivyo Mfumo huu sasa utasaidia kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi kunakoongeza uwazi na uwajibikaji wa vituo hivi”, Alisema



Akitoa maelezo ya awali Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Mradi wa Uimarishaji mifumo ya sekta za Umma (PS3) Bi Leah Mwainyekule amesema kuanzia Julai 1, 2017 Serikali inataraji kuanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya na sekta ya elimu kwa ngazi ya halmashauri hivyo mafunzo walioanza kuyatoa kwa ngazi ya taifa, halmashauri na kwa watumiaji wa mwisho katika mikoa Ishirini na Sita ya Tanzania Bara  yanalenga kusaidia kuongeza uelewa mpana na maarifa ya stadi za kuwezesha utendaji wa moja kwa moja kwa watumishi waliochaguliwa katika kituo kukabiliana na changamoto za utunzaji wa taarifa za fedha zinazowakabili

Aliongeza kwa kusema kuwa,  Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), wametoa mafunzo ya kina kwa wakufunzi 490 katika ngazi ya taifa na halmashauri nchini kote. Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mtwara, na Shinyanga, ambao nao sasa wanajukumu kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS.

Mfumo  huo wa FFARS ambao unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID una lengo la kuongeza ufanisi, hususan katika masuala mazima ya mapato, na ndio utakuwa mtatuzi wa malalamiko ya wananchi.


Akihitimisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela mbali na kuishukuru PSE kwa utoaji wa mafunzo amewaasa wataalamu waliohudhuria mafunzo hayo kuzingatia elimu wanayopewa ili kuongeza ufanisi katika kutimiza majukumu yao

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • WALENGWA TASAF WAASWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA VIKUNDI

    April 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.