• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MBUNGE ILEMELA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA AFYA LUMALA

Posted on: December 25th, 2018

Mbunge wa jimbo la Ilemela Mheshimiwa Daktari Angeline Mabula ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya Lumala kilichopo kata ya Ilemela na kilichogharimu takriban zaidi ya shilingi 40,490,000 kikiwa katika hatua ya kukamilika kwa Boma.

Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Lumala Mhe. Mabula amewapongeza wananchi hao kwa utayari wao wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kusogeza huduma muhimu kwa jamii kwa kukubali kuchangia kiasi cha shilingi 6,990,000 zilizotumika kwa ajili ya kukamilisha msingi wa kituo hicho kabla ya yeye kutoa matofali yote ya ujenzi wa boma la kituo hicho


‘… Niwapongeze sana wana Lumala ni mitaa michache sana ambayo wananchi wake wako tayari kujitokeza na kuchangia ujenzi wa miundombinu muhimu kama shule na zahanati, Wengi wanangojea Serikali ifanye na ndio maana mliponifata kunishirikisha sikusita kwa sababu niliona nguvu yenu …’ Alisema


Aidha Mheshimiwa Mabula amemuomba Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela kuhakikisha anamalizia hatua iliyobaki ya kupaua jengo hilo  kama wanavyoshirikiana katika kutekeleza miradi mingine ya maendeleo, Kwa sera ya utatu kwa maana ya wananchi kuchangia gharama za msingi, mbunge kujenga boma na manispaa kupaua.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ilemela Mheshimiwa Wilbard Kilenzi amemshukuru mbunge huyo kwa kuunga mkono jitihada za wananchi wa kata yake huku akimuomba kuendelea kutoa msukumo kwa ngazi  husika ili kituo hicho kiweze kufunguliwa kwa wakati uliokusudiwa.

Mara baada ya uzinduzi huo mheshimiwa mbunge aliendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi, changamoto, ushauri na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa viwanja vya michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono, na mpira wa pete vinavyojengwa eneo la Sabasaba katika kata hiyo. 



Announcements

  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2025 July 08, 2025
  • TANGAZO LA KAZI NAFASI YA UDEREVA DARAJA LA II June 04, 2025
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANAFUNZI WATAKIWA KUDUMISHA NIDHAMU

    July 30, 2025
  • WATAALAM WA MANISPAA YA ILEMELA WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA FFARS KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA

    July 28, 2025
  • WATAALAM WA MANISPAA YA ILEMELA WAHIMIZWA KUTUMIA MFUMO WA FFARS KATIKA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA

    July 28, 2025
  • MANISPAA YA ILEMELA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA MRADI WA GREEN AND SMART CITIES SASA

    July 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.