"Nitoe rai ya ukamilishaji wa miradi yote inayoendelea jimboni kukamilika kwa wakati".
Ni kauli iliyotolewa na Mhe.Dkt.Angeline Mabula ambae ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi wakati wa ziara ya kikazi akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea jimboni.
Sambamba na hilo ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi kuhakikisha kuwa maeneo yote yanayodaiwa fidia yanalipwa kuepusha migogoro ya ardhi pamoja na kuhakikisha taasisi zote za umma zinapimwa na kupata hati miliki.
"Pale panapostahili fidia zilipwe mapema ili kuepusha migogoro",amesisitiza Mhe.Mabula
Pamoja na hilo amepongeza kwa miradi mizuri na usimamizi mzuri wa miradi hiyo na kusisitiza kuendeleza ushirikiano uliopo ili Ilemela iweze kusonga mbele.
Mhe.Mabula ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi Ilemela za miradi wakati akiongea na wananchi wa Mihama kata ya Kitangiri alipofika kwa ajili ya kukagua ujenzi wa zahanati ya mihama inayojengwa kwa fedha za TASAF.
Mhe.Mabula amesema ,Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Samia imetoa kiasi cha shilingi Milioni 133 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Igogwe, shilingi milioni 173.5.kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya mihama, na shilingi milioni 74 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya igombe mwaloni.
Kuhusu suala la fidia Mhandisi Modest Apolinary ameeleza kuwa katika bajeti ya mwaka 2023/2024 kiasi cha shilingi Bilioni moja kimetengwa kwa ajili ya fidia pamoja na uthamini katika tasisi za umma huku akiahidi kutekeleza maelezo yaliyotolewa.
Mhe Angeline Mabula amekagua miradi ya ujenzi wa bweni shule ya sekondari Igogwe, ujenzi wa barabara ya Kahama kuelekea Shibula, barabara ya igombe mwaloni, zahanati ya Mihama pamoja na eneo la ujenzi wa zahanati mpya katika kata ya Kitangiri.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.