Katibu tawala wa Wilaya ya Ilemela Adv.Mariam Msengi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Mwl.Hassan Elias Masala amebainisha hayo wakati wa zoezi la ugawaji vyeti kwa washiriki wote wa zoezi la sensa ya watu na makazi lililofanyika mwaka 2022.
Jumla ya vyeti 1344 vimetolewa kwa makarani,makarani waandamizi, wasimamizi wa maudhui, wasimamizi wa TEHAMA na wakufunzi walioshiriki zoezi hilo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi mratibu msaidizi wa zoezi hilo Joseph Mrimi ametaja mafanikio ya zoezi ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa za idadi ya watu 509,687 na makazi katika kaya 127,507 kati ya kaya 121,542 zilizopangwa kuhesabiwa sawa na 104% ya lengo.
Adv.Msengi amesema mipango na mikakati ya kimaendeleo inapangwa kwa kuangalia idadi ya watu katika maeneo yao sambamba na huduma mbalimbali za kijamii nazo hutegemea idadi,jinsi na makundi.
"Matokeo hayo ya sensa yatachochea kasi ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Ilemela kwani tunahudumia watu tunaotambua idadi na makundi yao hii itapelekea mganyo wa uwiano sahihi wa huduma tunazotoa kwa wananchi wetu."Amesema Adv.Msengi
Nae Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi.Ummy Wayayu amepongeza timu nzima iliyoshiriki kufanikisha zoezi hilo la kitaifa.
Akihitimisha hafla hiyo Adv.Msengi ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega na uongozi wa Wilaya ya Ilemela mpaka kukamilika kwa zoezi la sensa kwa mafanikio makubwa.
"Nawashukuru wote mlioshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi, wananchi na makarani ama hakika mmeonyesha uzalendo mkubwa."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.