Mgeni rasmi Mhe. Hashimu Abdallah Komba, Mkuu wa wilaya ya Geita akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Geita Ndg. Martin Shigela leo tarehe 3Agosti 2025, amefungua rasmi maonesho ya Nanenane kanda ya ziwa Magharibi yanayofanyika viwanja vya Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela ambapo amesema kila mmoja anao wajibu wa kutembelea maonesho haya ya nane nane kwa ajili ya kujifunza lakini pia kujioatia bidhaa mbalimbali
“Kama ni mkulima utapata fursa ya kujifunza kilimo cha kisasa na Chenye tija na kama ni mvuvi pia unaweza kujifunza shughuli za uvuvi kwa teknolojia ya kisasa hivyo msiache kutembelea mabanda mbali mbali kujipatia elimu na uzoefu ” Alilisitiza muwakilishi huyo wa mgeni rasmi Mhe Komba
Akifafanua kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane Mwaka huu “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025” amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.