Leo tarehe 25 Julai, 2025 timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI ikiongozwa na Bi Zainab Manyike ambae ni mratibu wa mradi wa Green and Smart City SASA sambamba na Ndugu Essau Amenye mtaalam kutoka shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) ambao ndio wasimamizi wa mradi huu wamekutana na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi Ummy Wayayu
Lengo la ujio wao ni kupata uelewa namna mradi huu unavyotekelezwa ndani ya manispaa yake lakini pia namna Manispaa ya Ilemela ilivyofanikiwa kushirikiana na wadau wengine hususan VETA, FETA na SIDO kufanya uchambuzi wa vijana watakaopatiwa mafunzo ya kujengewa ujuzi katika vyuo hivyo kupitia ufadhili wa mradi wa Inclu- cities.
Aidha, wamempongeza Mkurugenzi na timu yake kwa namna wanavyoendesha shughuli za mradi lakini suala zima la ushirikishaji katika kutekeleza shughuli za mradi huu.
Nae Mkurugenzi Ummy amelishukuru Shirika la ENABEL kwa kuja na na mradi wa kuwajengea uwezo vijana kwani inawatengenezea msingi wa maisha, sambamba na hilo ametambua jitihada za mratibu wa mradi wa green and smart city Ndugu Ahmed Sakibu na kumtaka kuendeleza jitihada zake katika kuhakikisha mradi huo unakuwa na matokeo chanya kwa jamii ya Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.