Jumla ya vitabu 47,946 vimekabidhiwa leo tarehe na 25/04/2018 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Mkuu wa mkoa Mwanza Mhe. John Mongella kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Vitabu vilivyotolewa ni vya darasa la kwanza hadi la tatu ikiwa ni vitabu vya sanaa na mazingira (9620), afya na mazingira(9620), Kuandika(9620), Kusoma (9620), Maarifa ya jamii (4733) na kiingereza (4733).
Akikabidhi vitabu,Mhe. Mongella, amewaelekeza walimu wakuu wa shule zitakazopatiwa vitabu hivyo kuhakikisha wanavigawa kwa wanafunzi na sio kuvihifadhi stoo.
“Hatutegemei baada ya leo tukaenda shule tukakuta mkuu wa shule ameweka vitabu hivi stoo”, Alisema
Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa vitabu hivyo wapewe watoto wasome na isije ikatokea mtoto wa darasa la kwanza hadi darasa la tatu hajui kusoma wala kuandika kwani lengo la hivi vitabu ni kuondoa kitendawili cha kuwa na watoto wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewaelekeza waratibu elimu na wadhibiti ubora wa elimu ,kufuatilia ubora wa utoaji elimu, ufundishaji na ujifunzaji wa watoto.
Nao wanafunzi pamoja na walimu waliowawakilisha wengine wameishukuru serikali kwa kuwapatia vitabu hivyo ambavyo vitasaidia kuongeza ufanisi wa ufundishaji kwa walimu na ujifunzaji kwa walimu.
Afisa Elimu, vifaa na takwimu Ndugu Joseph Mrimi amesema kuwa vitabu hivi vitapunguza idadi ya upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi pamoja na kupunguza tatizo la kusoma,kuandika na kuhesabu
Vitabu hivi vitaanza kugawiwa kuanzia kesho tarehe 26/04/2018 katika shule 74 za msingi zilizopo kwenye kata 19 za Manispaa ya Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.