Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inaungana na Halmashauri nyingine nchini kuendesha zoezi la mafunzo ya ugawaji wa dawa (kinga tiba) kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo kichocho na minyoo ya tumbo.
Zoezi limeendeshwa katika vituo vinne vya shule ya msingi Baptist kata ya Nyamanoro shule ya msingi Ibeshi kata ya Nyakato, Igombe kata ya Bugogwa na kata ya Shibula ambapo wataalam wa afya, waalimu wa afya kwa shule za msingi wamejengewa uwezo kwa ajili ya kutoa dawa hizo katika vituo vyote vilivyopangwa kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 14 kuanzia kesho Alhamisi Novemba 23 hadi 24 ,2023.
Dawa(kinga tiba)hizo hazina madhara hivyo wazazi/walezi wanaombwa kuwapatia watoto chakula kabla ya kupewa kinga tiba hiyo na kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.