Manispaa ya Ilemela inaendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA katika kuimarisha ukusanyaji mapato katika sekta zote ambazo inajipatia mapato ya ndani kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Manispaa kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Afisa uvuvi wa Manispaa ya Ilemela Ivon Maha wakati akiwasilisha taarifa yake ya hali ya uvuvi katika manispaa hiyo kwa wataalam na madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakiongozwa na Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Mhe.Baraka Naibula Lupoli walipofanya ziara ya siku 1 kujifunza shughuli mbalimbali za ukusanyaji mapato katika Manispaa ya ilemela.
“..Matumizi ya mfumo wa TAUSI yameturahisishia utoaji wa leseni za uvuvi na malipo ya ada na tozo mbalimbali ,mfumo huu umetusaidia kupunguza mianya ya upotevu wa mapato katika sekta ya uvuvi...” amesema Maha
Theogenes Laurent ni Afisa mapato wa Manispaa ya Ilemela amesema Halmashauri hiyo imepanga kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 14.9 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo mpaka sasa imekusanya 40.31% ya lengo kwa mwaka huu wa fedha na inatarajia kufikia malengo kwa kuendelea kuboresha mifumo ya TEHAMA inayotumika katika kukusanya mapato sambamba na kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika kuleta uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa ulipaji ada za leseni na tozo mbalimbali kwa wakati.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe.Renatus Mulunga amesema uongozi wake unaendelea kuimarisha ushirikiano kwani ndio nguzo pekee ya kufanikisha mipango ya Manipaa yake.
Maeneo yaliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na Soko la kimataifa la samaki Mwaloni Kirumba lililopo kata ya Kirumba,Mwalo wa Kayenze ndogo uliopo kata ya Bugogwa na Stendi ya mabasi Nyamhongolo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.