“Ni matarajio ya tume huru kuwa kutokana na semina hii kila mmoja wenu atapata elimu na ujuzi wa kutosha kumuwezesha kutekeleza majukumu yake ili kufanikisha uboreshaji wa daftari la wapiga kura na mtaifanya kazi hii kwa ueledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili”
Kauli hiyo imetolewa na ndugu Egidy Teulas kwa niaba ya afisa mwandikishaji jimbo la Ilemela wakati akifungua mafunzo kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata (ARO Kata) siku ya Jumatano ya tarehe 14/08/2024
Ndugu Egidy amesema kuwa mafunzo hayao yamelenga kuwajengea umahiri wa kuwafundisha waandishi wasaidizi na waendeshaji vifaa vya bayometriki ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni.
Aidha ndugu Egidy amewasisitiza wanasemina juu ya umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji kwani vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika maeneo mengine nchini katika zoezi hili la uboreshaji
“Kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu nchini sambamba na hilo mnapaswa kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na tume ili muweze kuyafanyia kazi wakati wa zoezi litakapokuwa limeanza,”Amesema
Jaji Asina Omari ambae ni mjumbe wa tume huru ya taifa ya uchaguzi amewataka maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata kutambua kuwa wao ni viongozi na kazi yao kubwa ni kuratibu zoezi zima ndani ya kata zao pamoja na kuwaandaa wale wanaoenda kufanya kazi vituoni huku akiwasisitiza kutumia fursa hii ya mafunzo kuuliza maswali kusoma vitabu kufanya mazoezi ili mwisho wa siku zoezi liwe la mafanikio.
“Niwasihi mtumie muda wenu wa mafunzo vizuri sana ili nanyi muweza Kwenda kuwafundisha vizuri waandishi wasaidizi na waendeshaji vifaa vya bayometriki ngazi ya vituo”, amesema jaji Asina
Juma Maila Ngoloma (ARO Kata Nyakato) kwa niaba ya maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata ameahidi kuwa watakuwa makini na mafunzo hayo yatakayotolewa ili waweze kwenda kutoa elimu kwa wasaidizi wa ngazi za vituo.
Kabla ya kuanza mafunzo hayo maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata waliapa kiapo cha kujitoa katika vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri zoezi lililoendeshwa na hakimu mkazi mwandamizi mahakama ya wilaya ya Ilemela, Mhe Juma Dishon Opudo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.