Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza na wadau wa kilimo wametoa mafunzo kwa maafisa ugani wa Manispaa hiyo ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kilimo msimu huu.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Afisa kilimo wa mkoa Innocent Keya amesema ni muhimu kujiandaa vizuri na aina gani ya mazao tutakayoyalima ili yalete tija .
" ..Tuwakumbushe wakulima wetu kuchagua mazao yatakayoendana na hali ya hewa .."
Nae Meneja wa mamlaka ya hali ya hewa (TMA) kanda ya ziwa ndugu Augustino Nduganda amesema matarajio ya hali za mvua za vuli mwaka 2024 kwa Wilaya ya Ilemela ni za wastani hadi chini ya wastani kutoka 300 - 410 milimita.
Nduganda amefafanua kuwa inatarajiwa kwamba mtawanyiko wa mvua za vuli hautakuwa mzuri kwani utatawaliwa na vipindi vya ukavu wa siku 10 na kuendelea.
"...Hali ya unyevuunyevu wa udongo haitakuwa nzuri na inaweza kuathiri ukuaji wa mazao,tunawashauri wakulima wapande mazao yanayostahimili ukame na kukomaa kwa haraka..." Amesema Nduganda
Wadau wa mbegu Seed.Co,Taifa seed,BRAC walitoa maelezo ya mbegu bora walizonazo na kuwasihi wakulima kuomba ushauri wa uchaguzi bora wa aina za mbegu kulingana na uhalisia wa maeneo yao kwa kuangalia hali ya hewa, udongo n.k
Dr.Mshindo Msola ni mtaalam wa mbolea kutoka wazalishaji wa mbolea Minjingu amesema ni muhimu wakulima wafahamu kazi za mbolea na matumizi sahihi kuanzia wakati wa kupanda,kukuzia kwa viwango vya ubora ili wapate mavuno mengi zaidi.
Akihitimisha mafunzo hayo mwakilishi wa Afisa kilimo wa Manispaa ya Ilemela Vincent Mlongwa amesema Halmashauri inaendelea na utoaji elimu kwa wakulima wake katika kuhakikisha kuwa mabadiliko ya tabia nchi hayaathiri uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.