Maafisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wajengewa uwezo matumizi ya mfumo wa Wezesha portal unaotumika kwa ajili ya huduma zote za mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri nchini.
Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo Afisa TEHAMA wa Manispaa hiyo ndugu Peter George amesema shughuli zote kuanzia maombi ya mikopo zinapaswa kufanyika kwenye mfumo.
"Wezesha portal ni mfumo wa kielektroniki ulioundwa kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara kupata mikopo kupitia vikundi vyao,ni mfumo rahisi na unaokoa muda kwani unaweza kutumika mahali popote ." Amesema Peter
Florence Vedasto ni kaimu Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii amewataka maafisa hao kuwa makini kwa kila hatua ya matumizi ya mfumo katika kuhakikisha kuwa huduma bora inatolewa kwa wateja wote.
"..Wateja wetu ni vikundi vya wanawake,vijana na walemavu ni lazima tuelewe vizuri mfumo ili kuleta ufanisi katika zoezi zima la utoaji wa mikopo na itolewe kwa wanaostahili tu.."
Amina Bululu ni mratibu wa mikopo wa Manispaa ya Ilemela yeye amevitaka vikundi vyote vinavyotarajia kukopa kuelewa shughuli za uzalishaji wanazofanya au wanazotarajia kufanya kwani itawarahisishia kuleta uelewa wa pamoja lengo ikiwa kila mmoja afanye kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa pesa inarejeshwa kwa wakati.
|
|
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.