• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MAAFISA ELIMU KATA WATAKIWA KUZUTUMIA PIKIPIKI KWA KAZI ILIYOKUSUDIWA

Posted on: September 20th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mheshimiwa Daktari Severine Lalika amewataka maafisa elimu kata kuzitumia pikipiki  kwa kazi iliyokusudiwa.

Ametoa maelekezo hayo alipokuwa akikabidhi jumla ya pikipiki kumi na tisa kwa maafisa elimu kata wa kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mheshimiwa Rais Daktari John Magufuli.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mheshimiwa Lalika amemshukuru mheshimiwa Rais Daktari John Magufuli kwa kuleta pikipiki hizo zitakazosaidia kurahisisha utendaji kazi kwa maafisa elimu kata ili kunyanyua kiwango cha ufaulu na kusisitiza kuwa Serikali itakuwa makini kufuatilia matumizi sahihi ya pikipiki hizo.

‘… Nipende kuwaasa tu kuwa Serikali tuliyonayo ni makini hivyo ni lazima itakuwa inafuatilia matumizi ya vifaa hivi ambavyo vimeletwa kaajili ya manufaa ya watu wote wanaotegemea kupata huduma yenu …’ Alisisitiza


Aidha Mkuu wa Wilaya amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha kuwa  maafisa elimu kata ambao hawana elimu ya vyombo vya moto wanapata mafunzo hayo ili kuepuka ajali na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga amebainisha matarajio yake kutoka kwa maafisa hao  baada ya kukabidhiwa nyenzo hizo ikiwemo kuongezeka kwa kasi ya usimamizi wa elimu, ufuatiliaji wa elimu na kuongezeka kwa ufaulu huku akisisitiza kuwa watendaji wote waliokabidhiwa vyombo hivyo wanaowajibu wa kuvitunza, kuvilinda na kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa sambamba na kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wote watakaovitumia isivyostahili.

Sambasamba na hayo, Ndugu John Wanga alisema kuwa anaendelea kutambua juhudi za Mhe. Mbunge wa jimbo la Ilemela Angeline Mabula kwa  mchango wake katika kusaidia kuinua sekta ya elimu pamoja na sekta zingine jimboni.


Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilemela mheshimiwa Renatus Mulunga amewaasa watendaji hao kuwa waadilifu katika shughuli zao za kila siku ili kuinua taaluma wilayani humo kwani mafanikio yatakayopatikana hayatakuwa ya mtu mmoja isipokuwa ya jamii kwa ujumla wake.


Kwa niaba ya maafisa elimu kata, Mwalimu Lucas Mlesi ambae pia ni afisa elimu kata ya Pasiansi alihitimisha zoezi hilo kwa kuishukuru Serikali kwa kutoa pikipiki hizo huku akiahidi kuzitunza na kuzitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa.





Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • WALENGWA TASAF WAASWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA VIKUNDI

    April 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.