Jumla ya miti 100 imekabidhiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kuadhimisha wiki za mazingira duniani ambapo kilele chake hufanyika kila siku ya Tarehe 05 Juni.
Akikabidhi miti hiyo, mkuu wa Idara ya mazingira na usalama wa TBL kanda ya Mwanza Ndugu Method Marco, amesema kuwa wameamua kutoa miti hiyo ili kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani pamoja na kuunga mkono kauli mbiu ya mwaka 2022 isemayo Dunia ni moja tuimepandwa katika Shule ya Sekondari ya Buswelu iliyopo kata ya Buswelu.
Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika katika shule ya Sekondari ya Buswelu ikiwa ni moja ya shughuli zilizofanyika kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya mazingira duniani
Mhe. Sara Ngw’ani ambae ni Diwani wa kata ya Buswelu akiwa mgeni rasmi amesema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuitunza miti hiyo hadi hapo itakapokuwa mikubwa kwa kutambua umuhimu wake katika maisha ya viumbe hai
Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilemela Ndugu Phinias amesisitiza kwa kusema kuwa, utunzaji wa mazingira ni jukumu letu sote na kuwa ajenda ya serikali ni kufanya usafi na kulinda vyanzo vya maji kuzuia mmonyoko wa udongo na upandaji wa miti ili kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.