Halmashauri ya Ilemela kupitia idara ya afya kitengo cha lishe inaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii Ilemela kwa lengo la kuleta uelewa wa pamoja wa namna ambavyo jamii inaweza kuwa salama kiafya kupitia lishe bora.
Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo kwa watumishi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Ilemela Mratibu wa lishe wa Manispaa ya Ilemela Bi.Pili Khassim amesema ni wakati wa jamii nzima kuona umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa afya zao kwa lishe bora.
"Kwa kutumia mchanganyiko wa chakula chenye virutubisho vyote na uwiano sahihi tunaweza kuepuka magonjwa mbalimbali ikiwemo baadhi ya aina ya saratani, magonjwa ya moyo na kisukari."
Joyce Albert ni Afisa lishe Wilaya ya Ilemela yeye anasisitiza juu uzito wa mwili ulio sahihi kwa kula mboga mboga na matunda kwa wingi na kuepuka vyakula vya wanga na mafuta kwa kiasi kikubwa ili kuepuka uzito uliozidi na kukithiri viwango vinavyohitajika.
Bi.Rehema ni mmoja wa watumishi wa TAKUKURU Ilemela yeye anatoa shukrani kwa kitengo cha lishe Ilemela kwa kazi nzuri wanayoendelea nayo ya kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali ya lishe.
" Elimu juu ya siku 1000 za mtoto ni ngeni kwangu ila imenipa uelewa mkubwa sana juu ya lishe bora tangu mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.Ni kitu kizuri kiendelee kitaokoa wengi."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.