Makamu wa Rais Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango amesema ni wajibu wa jamii nzima kutambua umuhimu wa lishe bora kuanzia hatua za awali za ukuaji wa mtoto kwani ili taifa liendelee linahitaji watu wenye uelewa mpana juu ya mambo mbalimbali ya msingi.
Akizungumza wakati akitoa salamu kwa wananchi wa kata ya Buswelu eneo la Buswelu senta akiwa njiani kuelekea wilaya ya Magu kikazi Dkt Mpango ameitaka jamii kuhakikisha kuwa kina mama wajawazito wanapata lishe bora tangu kipindi cha ujauzito hadi kukua kwa mtoto.
Akijibu hoja ya uwepo wa chakula mashuleni kwa baadhi ya wananchi wanayoikataa Dkt.Mpango amesema ni wajibu wa wazazi kuwahudumia watoto wao kupata mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo chakula hivyo suala la watoto kula wakiwa shuleni ni haki yao.
“ Wazazi/walezi na walimu wakae pamoja wakubaliane namna ya kuliendesha suala la chakula shuleni kwa utaratibu mzuri wenye manufaa kwa wote.” Amesema Dkt.Mpango
Nae Waziri wa maji Mhe.Juma Aweso amewahakikishia wananchi wa Ilemela huduma ya maji kuboreka zaidi kwa kuwataka Idara ya maji kumaliza haraka mradi wa maji wa tenki la Buswelu na maji kuanza kutoka mara moja.
“ Pesa ipo ishatolewa kukamilisha mradi,natoa wiki sita kukamilisha mradi huu kwa watu wa MWAUWASA,ikitokea mtu amezingua tutazinguana.” Amesema Mhe.Aweso.
Aidha Mhe.Mpango amewashukuru wana Ilemela na wananchi wote kwa mapokezi mazuri na kuwasihi kuacha kukumbatia tamaduni za kigeni zisizo na manufaa kwetu kama vile kuruhusu mambo ya ushoga na usagaji.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.