Kuelekea hafla ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 vikundi 60 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambao wamefuzu kupatiwa mikopo hiyo inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri vimepatiwa elimu ya matumizi sahihi ya mikopo.
Akizungumza wakati wa zoezi ya utiaji saini mikataba ya mikopo hiyo kwa vikundi vilivyokidhi vigezo vya kupata mkopo Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Mohammed Atiki amesema ni utaratibu wa kawaida kutokana na miongozo ya utoaji mikopo ya serikali inayolenga kuwepo kwa makubaliano hai yatakayolinda pande zote mbili mkopeshaji na mkopaji.
".. Endapo wakopaji mtashindwa kulipa mtawajibishwa kulingana na makubaliano ndani ya mkataba .."
Akitoa ufafanuzi wa vipengele mbalimbali ndani ya mkataba huo mwanasheria wa Manispaa hiyo Adv.Mariam Omary amesema kuwa dhamana ya mikopo hiyo ni wanakikundi wenyewe hii ni kulingana na mkataba unavyofafanua.
".. Endapo mwanakikundi au kikundi kitashindwa kurejesha mkopo wanakikundi wote watawajibika.."
Adv.Mariam ameainiasha sababu mbalimbali za kuweza kuvunjika kwa mkataba huo ikiwemo mkopaji kushindwa kufanya matumizi ya mkopo kwa usahihi,mkopaji kufanya jambo lolote litakalovunja uaminifu na imani ya mkopeshaji.
Happiness Peter ni miongoni mwa wanakikundi katika kikundi cha Upendo kilichopo kata ya Nyakato wanaojishughulisha na ushonaji kwa niaba wanakikundi wenzake wameahidi kuwa mfano bora kwa kutekeleza mradi wao kwa ubora zaidi na kufanya marejesho kwa wakati.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.