“Hakuna jambo la muhimu na msingi kama watumishi kusimamia maadili na misingi ya utumishi wa umma”
Hayo yamesemwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Ngusa Samike alipokuwa akiongea na watumishi wa makao makuu ya Manispaa ya Ilemela baada ya kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayoendelea.
Amewasisitiza pia kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu pamoja na kusimamia misingi ya kanuni za utumishi kwani ndizo ambazo zitawalinda katika utelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Pamoja na hayo amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela kwa usimamizi mzuri wa miradi ndani ya kipindi kifupi ambacho amehudumu katika manispaa hii huku akiwapongeza TARURA kwa upande wa Ilemela katika usimamizi wa miradi ya barabara na kuwataka kuendeleza jitihada hizo .
Halikadhalika akiongea na watumishi hao ameihimiza Idara ya usafishaji kuhakikisha kuwa wanawasimamia wananchi kufanya usafi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutunza uoto wa asili.
Akiwa katika manispaa ya Ilemela,Ndugu Samike ametembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya kahama kuelekea kabusungu, ujenzi wa tanki la maji lililopo Buswelu pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Masanza.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.