"KATEKELEZENI KAZI HII KWA UELEDI”: UMMY WAYAYU
Wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa kutathmini matokeo ya awamu ya nne ya mradi wa kupunguza umaskini Tanzania (TRPIV) wametakiwa kutekeleza kazi iliyopo mbele yao kwa ueledi na umakini wa hali ya juu ili ikalete matokeo chanya.
Rai hiyo imetolewa na mgeni rasmi Bi Ummy Wayayu ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela wakati akifunga mafunzo ya wasimamizi na wadadisi hao.
" Ni imani yangu kuwa kutokana na mafunzo mliyopatiwa, na umahiri wenu najua mtaifanya kazi hii kwa umakini na ueledi wa hali ya juu ili ikalete tija", amesema Bi Ummy Wayayu.
Aidha pamoja na hilo Bi Ummy ametoa wito kwa viongozi wa mitaa na vijiji na wananchi kutoa ushirikiano wa kila hali kwa watendaji wa ofisi za Taifa ya Takwimu pindi watakapofika katika maeneo yao kwa lengo la kukusanya taarifa za utafiti.
Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ndugu Japhet Boaz amesema kuwa madhumuni ya kutathmini mradi huu ni kuangalia ni kwa namna gani uwekezaji wa serikali umeleta tija katika kuwahudumia wananchi wake ili kuweza kuondokana na hali duni na hivyo kuweza kuboresha maisha yao.
Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uelewa wasimamizi na wadadisi katika kukusanya takwimu za utafiti wa kutathmini matokeo ya mradi huu wa TPRP-IV.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.