Hivi karibuni kampuni ya simu ya tigo ilikabidhi kompyuta 10 kwa Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu na ukusanyaji wa mapato katika zahanati na vituo vya afya.
Kompyuta hizi zitasaidia katika kuboresha taarifa mbalimbali za vituo vya afya pamoja na zahanati halikadhalika pamoja na kuboresha ukusanyaji wa mapato na kuzuia/kuepusha upoteaji wa mapato ya Halmashauri hasa katika kipindi hiki tunapotoka katika mfumo wa analogia kuelekea digitali.
Kampuni ya Tigo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika manispaa ambapo hadi sasa wameshatoa madawati kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kuboresha sekta ya mawasiliano katika shule za manispaa ya ilemela kwa kutoa simu za mtandao wa tigo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.