Ikiwa ni robo ya pili kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 waheshimiwa madiwani wakiwa katika kamati wanazohudumu wameweza kutembelea na kukagua miradi inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Kwa upande wa kamati ya Huduma ambayo walitembelea miradi ya ujenzi wa madarasa lengo haswa ikiwa ni kufuatilia ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali ambayo inahusika na utoaji wa huduma za kijamii.Katika ziara ya robo ya pili wajumbe wa kamati hii waliweza kukagua ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za sekondari ikiwa ni pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya. Walipata pia fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wakinamama kwa ajili ya kujifungulia lililopo zahanati ya nyakato.Pia waliweza kukagua soko lililopo nyasaka kwa ajili ya kuangalia namna ambayo wataweza kuboresha miundominu ya soko hili ili liweze kuboreshewa miundombinu kwa ajili ya kutumika na wafanyabiashara. Pamoja na kufanya ukaguzi huo walisisitiza suala la ukamilishaji wa miundombinu ya madarasa ili kuweza kuendana na agizo la Waziri Mkuu huku wakisisitiza ukamilishaji wa miradi mbalimbali ili kuweza kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Kamati ya Mipangomiji nayo ilipata fursa ya kukagua miradi ambayo inasimamiwa na kamati hiyo ikihusiana na suala la zima la ujenzi, ardhi na mipangomiji. Wakiwa katika ziara hiyo waliweza kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Stendi ya mabasi na uegesheji wa malori Nyamhongolo ambapo walipongeza na kushauri kuwa ufuatiliaji ufanyike ili pesa iletwe kwa wakati kwa ajili ya kuweza kukamilisha ujenzi huo kwa wakati. Aidha waliweza kufuatilia masuala ya migogoro ya ardhi katika manispaa na kuwataka wataalamu wa Idara ya Mipangomiji wanatatua migogoro hiyo ili kuondoa kero kwa wananchi
Ziara za robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zilihitimishwa na Kamati ya Fedha ambapo wajumbe wa kamati hiyo waliweza kukagua mialo katika Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kusikiliza changamoto za wavuvi ikiwa uvuvi ni chanzo kikuu cha mapato cha Ilemela, aidha waliweza kukagua maendeleo ya ukarabati wa mzani wa kupimia magari yanayopitisha mazao ya uvuvi uliopo mwaloni kirumba.Kamati hiyo pia iliika kukagua maendeleo ya ujenzi ya mabweni mawili ya wasichana katika shule za sekondari Bwiru wasichana na Buswelu huku wakiagiza kuhakikisha kuwa mabweni yanakamilika ili kuweza kuanza kutumika.
Ziara hizi za kamati za kudumu hufanyika katika kila robo na lengo kuu ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Halmashauri kwani kamati hizi za kudumu zinao wajibu wa kuishauri halmashauri kutengeneza malengo yanayozingatia matakwa ya Miji na kuchukua, hatua ambazo zitaonekana zinafaa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Aidaha kamati hizi hushauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya Sera muhimu pamoja na kuishauri Halmashauri kufanya maamuzi juu ya utoaji wa huduma kulingana na rasilimali zilizopo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.