Wajumbe wa kamati ya uongozi ya TASAF taifa wamefanya ziara ya siku moja kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) ndani ya Manispaa ya Ilemela.
Akiwa kwenye mradi wa walengwa wa mtaa wa Kayenze ndogo wa ufugaji samaki kwa teknolojia ya vizimba uliogharimu takribani milioni 34,unaotekelezwa eneo la Kamanga kiongozi wa msafara wa wajumbe hao Dkt. Naftal Ng'ondi amesema elimu ya ufugaji wa samaki iendelee kutolewa kwa wananchi kwani inaendelea kuonyesha tija kubwa kwa watu wanaoitumia ipasavyo.
".. Lengo kuu la mradi huu ni kuongeza kipato na kuondoa umaskini ambalo ndilo lengo la TASAF,tunatamani wananchi wengi watoke kwenye umaskini.Nawapongeza sana kwa kubuni mradi huu.."
Aidha kamati hiyo imetembelea mradi wa ujenzi wa zahanati ya Mihama iliyopo ndani ya kata ya Kitangiri ambao tayari umeanza kufanya kazi.
".. Natoa rai kwa jamii ya Mihama na maeneo jirani kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wanafika zahanati kupata chanjo na huduma zingine za afya.."
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi.Ummy Wayayu amewataka wana Ilemela kuwa walinzi wa miundo mbinu yote iliyopo zahanati ya Mihama ili idumu itumike kwa kizazi cha sasa na baadae .
Paul Otieno ni katibu wa mazingira CCM kata ya Kitangiri yeye anasema zahanati hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii huku akitoa ombi la maboresho ya barabara inayoelekea katika zahanati hiyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.