Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa Mhandisi Modest Apolinary imekagua miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Halmashauri hii.
Miradi iliyokaguliwa ni mitano yenye thamani ya Tsh Bilioni 3.16 ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika kituo cha Afya Buzuruga, ujenzi wa shule mpya ya msingi Kangaye, ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum, ukamilishaji wa matundu 20 katika shule ya msingi lukobe pamoja na ujenzi wa jengo la utawala.
Kati ya Miradi hiyo miradi minne inagharamiwa na halmashauri kupitia fedha za mapato ya ndani na mradi mmoja wa jengo la utawala unagharamiwa na fedha kutoka serikali kuu.
Mkurugenzi Modest ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa wodi ya mama na mtoto katika kituo cha Afya Buzuruga ukamilike kwa wakati uliokusudiwa, kuhakikisha mapungufu yaliyobainishwa katika miradi hiyo kufanyiwa marekebisho pamoja na hayo amezipongeza idara zinazosimamia miradi hiyo kwa kazi nzuri.
Alihitimisha kwa kuwapongeza wakuu wa idara kwa utekelezaji mzuri wa miradi inayoendelea kushauri kuwa ziara ya kamati ya menejimenti kufanyika kila mwezi na sio kusubiri ziara za kila robo mwaka ili kuweza kufuatilia fedha za ndani zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ndani lakini pia fedha kutoka serikali kuu
Ziara hii ya ukaguzi ni ya robo ya mwaka hufanyika kila baada ya robo ya mwaka kukamilika na hii ikiwa ni ziara ya robo ya kwanza Julai-Septemba mwaka 2022/2023.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.