Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga ameitaka kamati ya lishe ya halmashauri ya Manispaa Ilemela kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano, mama wajawazito na wanawake ili kupunguza na kuzuia tatizo la udumavu.
Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa robo mwaka wa kamati hiyo na kuwataka wajumbe kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuifikia jamii, na kutoa elimu yenye kuzingatia lishe bora na umuhimu wake kwa watoto, wanawake, mama wajawazito na jamii kwa ujumla.
‘… Kuna shida ya lishe katika jamii na bado kamati haijafanya vizuri katika kutimiza jukumu hili, hivyo nawakumbusha jukumu kubwa la kamati hii ni kwenda kuhamasisha umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa watoto, wanawake, mama wajawazito na jamii kwa ujumla wake ili wasidumae” ,Alisisitiza Mkurugenzi.
Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilemela Daktari Florian Tinuga alisema kuwa Manispaa ya Ilemela itahakikisha inakuwa na mikakati endelevu yenye lengo la kushawishi jamii juu ya kuzingatia lishe bora kupitia timu jumuishi yenye wataalamu kutoka idara mbalimbali ili kupunguza changamoto zinazosababishwa na lishe duni huku akitaja zaidi ya watu 402,175 wanaorajiwa kufikiwa kwa kata zote 19 za wilaya hiyo na mitaa yake 171 kwa kushirikiana na vikundi vyenye ushawishi,asasi nyengine zisizo za kiserikali na viongozi wa maeneo husika.
Mkutano huo ulienda sambamba na utambulisho wa mradi wa ‘MTOTO MWEREVU’ unaotarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya Manispaa Ilemela wenye lengo la kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Geita na Shinyanga kwa ufadhili wa watu wa Uingereza (UKaid ) kupitia asasi isiyo ya kiserikali ya IMA World Health.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.