Kamati ya lishe imekutana na kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe katika Manispaa ya Ilemela ambapo Afisa Lishe Bi paulina Machango aliwasilisha taarifa hiyo akiainisha shughuli mbalimbali ambazo zimetekelezwa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 Januari – Machi
Taarifa juu ya kadi alama ya lishe ikiwa na viashiria 12 ambavyo vinatumika kufuatilia utekelezaji wa afua za lishe iliwasilishwa ambapo wajumbe kwa pamoja walikubaliana kuwa nguvu zaidi iongezwe katika utoaji elimu ya lishe kwa jamii ya Ilemela.
Aidha Bi Pauline Machango aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/23 ambapo alizitaja shughuli mbalimbali zilizotekelezwa katika kipindi hicho baadhi yake ni; kutoa elimu ya lishe kwa wazazi/walezi katika kata tatu za Nyamhongolo, Bugogwa na Ilemela, usimamizi shirikishi pamoja na uhakiki wa ubora wa takwimu za viashiria vya lishe kwa vituo vya kutolea hudu,a za afya ya mama na mtoto, ununuzi wa chakula dawa kwa ajili ya kutibu watoto wenye umri chini ya miaka 5 wenye utapiamlo pamoja na shughuli nyingine.
Kupitia kamati hiyo ya lishe, iliwasilishwa taarifa ya utekelezaji wa mpango wa chakula mashuleni ambapo Mkuu wa divisheni ya Elimu Msingi na awali Mwalimu Busungu, akiwasilisha taarifa ya utoaji chakula kwa shule za msingi ilemela amesema kuwa hadi kipindi hiki jumla ya shule 52 kati ya 76 za serikali zimeanza kutoa lishe shuleni na kuahidi hadi kufikia mwisho wa mwezi wa tano shule zote zinatoa lishe, Kwa upande elimu sekondari Mwalimu Mrimi alisema kuwa jumla ya shule 10 kati ya 32 za serikali zinatoa chakula
Wajumbe walisisitiza juhudi zaidi zifanyike kuhakikisha shule zote zinatekeleza mpango wa chakula mashuleni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu utoaji wa chakula katika shule zote za msingi na sekondari kwa kuhakikisha unafanyika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha pia chakula kinachotolewa kiwe ni kilichoongezwa virutubishi ili kuboresha afya za wanafunzi
Katika mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri kupitia idara ya afya imetenga kiasi cha shilingi milioni 85.8 kutoka mapato ya ndani hii ni kulingana na idadi ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwa ajili ya kutekeleza shughuli za lishe na hadi sasa utekelezaji wa shughuli za lishe umefikia asilimia 77.5
PICHA MBALIMBALI ZA KIKAO CHA KAMATI YA LISHE ILEMELA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.