Kamati ya kudhibiti UKIMWI ya Manispaa ya Ilemela ilifanya ziara kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali ambazo zimetekelezwa katika kipindi cha robo ya kwanza (July-septemba) kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Ziara hii ilihusisha kutembelea, kukagua na kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za udhibiti na mapambanao ya ugonjwa wa Ukimwi, taarifa za Upimaji na Unasihi, Tiba na huduma za CTC .
Maeneo waliyotembelea ni pamoja na kituo cha Afya Karume kilichopo kata ya Bugogwa, Zahanati ya Kirumba iliyopo kata ya Kirumba, Kikundi cha wanaharakati JABOYA kinachojihusisha na shughuli za udhibiti Ukimwi cha kata ya Bugogwa na kikundi cha kina mama cha Huruma Women Group cha kinachofanya shughuli zake za udhibiti Ukimwi kwa wilaya ya Ilemela na Nyamagana
Wajumbe wa kamati hiyo wameshauri kuwa idadi ya majengo ya kutolea huduma iongezwe, uwepo wa uhakika wa upatikanaji dawa kwa wagonjwa wa VVU, Manispaa ya IlemelaUKIMWI
na pia kuhakikisha kunakuwepo upatikanaji wa vifaa vya kutolea huduma kwa CTC.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.