KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA ILEMELA YAZITAKA TAASISI BINAFSI KUWASILISHA TAARIFA ZA UTENDAJI KAZI WAO
Mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya Manispaa ya Ilemela Mheshimiwa Shaaban Maganga amezitaka taasisi binafsi zinazofanya kazi ndani ya Manispaa ya Ilemela kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zao za kila siku. kwa serikali
Maagizo hayo yalitolewa wakati wa ziara ya kamati hiyo ya robo ya tatu iliyohusisha upokeaji wa taarifa za mpango wa jinsia na ukimwi, upimaji wa Virusi vya Ukimwi , tiba, matunzo na mpango wa kudhibiti ukimwi kutoka katika mashirika yasiyo ya kiserikali ya kivulini , Busega Microfinance Bureau na kituo cha kutolea huduma za upimaji na vvu kilichopo ndani ya kituo cha afya cha Buzuruga
Akizungumza katika ziara hiyo Mheshimiwa Maganga amesema kuwa ipo haja kwa taasisi zote zinazofanya kazi ndani ya wilaya yake kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zake za kila siku kwa serikali lengo likiwa ni kuzisimamia na kuhakikisha zinatekeleza malengo ya kuanzishwa kwake sambamba na kuzuia vitendo vya uvunjifu wa sheria na taratibu walizojiwekea
“Niziombe taasisi zote zinazofanya kazi ndani ya wilaya yetu kuwa na utaratibu wa kuwasilisha taarifa za utendaji wao wa kazi za kila siku, lengo sio baya hii itasaidia kujua uhalisia wa wanachokifanya na uwajibikaji wao kwa jamii mana kuna nyengine hazitekelezi yale yaliyokusudiwa kwa kuanzishwa kwake na madhara yanapotokea mwenye taasisi anakuwa hayupo ila serikali ipo nakubeba hasara zote” Alisema.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa manispaa ya Ilemela Daktari Wilfred Rwechungura aliongeza kwa kusema kuwa kuwa taasisi nyingi zimekuwa zikifanya shughuli zake kwa mazoea bila kufuata taratibu na sheria za serikali kunakosababisha migongano na sintofahamu kwa jamii
“Zipo taasisi zinatoa elimu ya mambo ya uzazi kwa watoto je wanatumia mtaala gani? Inawezekana badala ya kupambana na maambukizi ya virusi vya ukimwi tukawa ndo tunachochea maambukizi mapya kwa kuwapa elimu yakutosha na mwisho wakaanze kujaribu” alisema.
Akihitimisha ndugu Methew Shadrack mkurugenzi wa kituo cha Busega Microfinance Bureau Limited kilichopo Kiloleli ameishukuru kamati kwa kutembelea kituo chake mbali na kuahidi uwasilishaji wa taarifa za utendaji wake wa kazi amesema kuwa ataendelea kushirikiana na serikali pamoja na kufata taratibu zote katika kuifikia dhamira ya serikali ya kuletea maendeleo kwa wananchi
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.