KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI YAITAKA HALMASHAURI YA ILEMELA KUVITAMBUA VITUO VYA WATOTO YATIMA Kamati ya Huduma za uchumi, Afya na Elimu, imeitaka Halmashauri kuvitambua vituo vyote vya watoto yatima na kuviweka kwenye bajeti kwa ajili ya kuvisaidia. Hayo yalisemwa wakati wa tathmini ya ziara iliyofanyika tarehe 17/02/2017 kwa ajili ya kubainisha na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake. Halikadhalika walishauri kuwa shule zote zilizofanya vizuri kupongezwa ili kutoa motisha kwa wengine waweze kufanya vizuri huku wakiweka mikakati mbalimbali katika kuimarisha utoaji wa elimu na kuongeza ufaulu ndani ya wilaya hiyo, sambamba na kuzisaidia shule zote zilizofanya vibaya ili ziweze kufanya vizuri kwa awamu nyingine. Pamoja na hayo walitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuyakumbuka maeneo yaliyo pembezoni na halmashauri kama vile visiwa vya bezi vilivyopo kata ya Kayenze kwa kuyapatia huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kuboresha maisha ya wananchi waishio maeneo hayo. Ziara hiyo iliongozwa na Mheshimiwa Sara Ng’hwani ambae ni Mweneyekiti wa Kamati ya huduma za uchumi ilitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo Zahanati (Luhanga), Vituo vya Afya(Karume), Shule za Msingi(Bezi) na sekondari(Bujingwa, Pasiansi) Mialo ya Ziwa Viktoria(Igombe ndogo) na kuhitimisha ziara yake Visiwa vya Bezi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.