KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI ELIMU NA AFYA YAFANYA UFUATILIAJI WA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAENDELEO
Kamati ya huduma ya uchumi elimu na afya ya manispaa ya Ilemela imefanya ziara kwa ajili kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika manispaa kwa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Ziara hiyo ililenga kutembelea na kukagua namna kilimo cha mabanda (green house) kinavyoendeshwa katika eneo la Nyamhongolo pamoja na kukagua hali ya utoaji huduma katika zahanati za Kirumba na kitangiri halikadhalika ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa Sarah Ng’wani amesema kuwa ni wajibu kwa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo ya pamoja kwa jamii
“Sera ya Serikali ni kushirikisha wananchi katika kufanikisha miradi ya maendeleo serikali inapofanya nusu na mwananchi nae achangie nusu iliyobaki hatutaunga mkono mradi wowote wa maendeleo ambao hauna ushiriki wa wananchi, tuwaombe waanze kuchangia shughuli za kimaendeleo na patakapobakia halmashauri itamalizia”, Alisisitiza
Nae ndugu Amosi Zephania akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa amesisitiza kuwa Serikali haitawavumilia wananchi wanaokwamisha kwa makusudi miradi ya maendeleo sambamba na kuwaomba viongozi wa maeneo yenye changamoto ya uelewa wa wananchi katika kuchangia kushirikisha wataalamu wa manispaa katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchangia maendeleo
Kamati hiyo pia imedhamiria kuimarisha miradi ya kilimo itakayotoa ajira nyingi kwa vijana katika kukabiliana na tatizo la ajira sambamba na utatuzi wa changamoto zote za miradi inayoendelea ili kuwaletea wananchi wa Ilemela maendeleo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.