Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inaendelea na ufuatiliaji na usimamizi wa matumizi bora ya fedha katika miradi mbalimbali inayoendelea wilayani humo .
Hayo yamethibitishwa kupitia kamati ya huduma,elimu na afya ya Ilemela inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Andrew Nginila ambae pia ni diwani kata ya Nyamhongolo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa wodi tatu wenye gharama ya kiasi cha shillingi milioni 500 mpaka ukamilifu wake katika hospitali ya Wilaya ya Ilemela .
Mheshimiwa Nginila amesema ni muhimu kwa wodi hizo kukamilika kwa wakati kwani tayari wakazi wa Isanzu na maeneo mengine ya jirani wameanza kunufaika na uwepo wa huduma hizo.
“Kazi hii ikamilike kwa wakati kama mhandisi ulivyoahidi ili ikalete tija na ufanisi uliokusudiwa,ni wajibu wetu kusimamia fedha hizi kwani tunajiridhisha kuwa wananchi wetu wanakwenda kupata kilicho bora na wanachostahili.”amesema
Akizungumza walipokuwa katika mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya sekondari Masanza Mchumi wa Manispaa ndugu Mophen amesisitiza kuboreshwa kwa usimamizi na ufatiliaji wa fedha zote za miradi ya umma.
“Tunaupongeza uongozi wa kata ya Kahama kwa kazi nzuri wanayoendelea nayo ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa,maabara mbili na ofisi tatu kwa nguvu za wananchi,hapa halmashauri imetoa milioni 69 tu kwa ajili ya ukamilishwaji wa ujenzi wa majengo haya, ambapo kweli tunaona thamani ya fedha kwa macho.” Amesema
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa nguvu ya wananchi mpaka hatua ya boma na ukamilishwaji wake na manispaa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 15 sambamba na mradi wa jengo la huduma za uzazi katika zahanati ya Nyamhongolo.
Kamati hiyo imesisitiza kipaumbele cha matumizi ya mafundi wakazi katika maeneo husika ya miradi ikiwa ni moja ya njia ya kupunguza gharama za ujenzi na kupata kitu kizuri kwa bei nafuu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.