Kamati ya fedha ikiongozwa Mwenyekiti Mhe.Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela imefanya ziara ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 .
Lengo la ziara hii ni kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kupitia fedha kutoka serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri.
Miradi ya takribani shilingi Bilioni 24.48 ilikaguliwa na kamati hii ikijumuisha ya sekta ya afya , elimu na barabara
Kwa upande wa sekta ya elimu, miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Shibula,Lumala na Bugogwa shule ya msingi, kwa upande wa sekta ya afya miradi 2 ilikaguliwa ambayo ni kituo cha afya karume ukamilishaji wa jengo la kufulia na ujenzi wa zahanati ya nyambiti na sekta ya barabara walikagua ujenzi wa barabara Nyamadoke hadi Nyamhongolo.
Wajumbe wa kamati walipongeza kwa jitihada zinazoendelea za utekelezaji wa miradi huku wakihimiza itekelezwe kwa wakati kwa kuzingatia thamani ya fedha.Kwa upande wa ujenzi wa barabara ya Nyamadoke wameelekeza maeneo korofi ya barabara hiyo yafanyiwe ukarabati wakati ujenzi ukiendelea.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.