Kamati ya fedha na uongozi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikiongozwa na Kaimu mwenyekiti wake Mhe. Godlisten Kisanga imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Buswelu - Nyamadoke - Nyamhongolo yenye urefu wa kilomita 9.5 ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 31 pamoja na mradi pacha wake wa barabara ya Buswelu- Busenga- Coca cola zenye jumla ya urefu wa kilomita 12.8, Ujenzi wa vyumba vya madarasa vitano pamoja na matundu nane ya vyoo katika shule ya sekondari Nyamhongolo mradi uliogharimu shilingi milioni 139 kutoka serikali kuu.
Ujenzi wa jengo la huduma za mionzi katika kituo cha Afya Buzuruga unaotarajiwa kugharimu shilingi milioni 65 fedha kutoka mapato ya ndani ya Manispaa,ujenzi vyumba vya madarasa 7 na ukamilishaji wa vyumba vitatu pamoja na ununuzi wa viti na meza 400 katika shule ya sekondari Nyasaka kwa gharama ya shilingi milioni 200 fedha kutoka serikali kuu sambamba na jengo la utawala kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara unaofadhiliwa na benki ya Dunia kupitia mpango wa uboreshaji miundo mbinu ya miji Tanzania (TACTIC).
Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi yote na kuzidi kusisitiza uadilifu katika matumizi ya fedha za serikali kwa miradi inayoendelea na kuwataka wataalam kukamilisha kwa wakati kwa manufaa ya umma.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.