Kamati ya fedha na Uongozi ikiongozwa na Naibu Meya Mhe.Manusura Lusigaliye imefanya ziara ukaguzi wa miradi ya maendeleo robo ya nne lengo ikiwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ambayo inatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani pamoja na fedha kutoka serikali Kuu.
Wajumbe wa kamati ya fedha wamepongeza kwa miradi hiyo na wakishauri kwa miradi ambayo haijakamilika kukamilika ndani ya muda uliopangwa huku wakielekeza mapungufu yaliyojitokeza kwenye barabara zinapopita daladala katika stendi ya Nyamhongolo kufanyiwa kazi.
Jumla ya miradi sita ambayo ni shule mpya mbili zinazojengwa kwa fedha za BOOST, ujenzi wa Barabara za Hospitali ya Wilaya na Stendi ya Nyamhongolo, Maabara katika shule ya Sekondari Kabuhoro, pamoja na ujenzi wa bweni na vyumba 3 vya madarasa katika shule ya sekondari ya wasichana Bwiru miradi yote hiyo ikigharimu Takriban Shilingi Bilioni 2.69 fedha za Serikali Kuu na mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.