Kamati ya kusimamia miradi ya BOOST ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa idara ya elimu msingi Manispaa ya Ilemela Mwl.Marco Busungu imefanya ziara ya kutembelea maeneo ambako miradi itatekelezwa kupitia programu ya BOOST mwaka 2023/2024.
Akiwa kata ya Bugogwa Mwl.Busungu amesisitiza kamati hiyo kuangalia maeneo yatakayokuwa rafiki kuweka miundo mbinu mbalimbali ya shule za msingi na awali sambamba na urahisi wa kufikika kwake kwa majira yote kwa kuzingatia miongozo ya programu hiyo.
Ikumbukwe kwamba mnamo Mwezi Juni 2024, Manispaa ya Ilemela ilipokea jumla ya kiasi cha shilingi milioni 507 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu ya awali na msingi kwa kata za Shibula na Bugogwa.
Katika fedha hizo Tshs.351.5 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mkondo mmoja na Tshs.155.5 ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali ya mfano, vyumba vitatu vya madarasa na matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Kayenze ndogo iliyopo kata ya Bugogwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.