• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

JAMII YATAKIWA KUWA NA MTAZAMO CHANYA DHIDI YA MEMKWA

Posted on: October 26th, 2024

Jamii imetakiwa kuwa na mtazamo chanya dhidi ya mpango wa elimu ya msingi kwa watoto walioikosa MEMKWA ili kutoa fursa ya wanafunzi wasiokuwa katika mpango wa kawaida kunufaika na programu hiyo.

Rai hiyo imetolewa na mwakilishi wa mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni afisa elimu msingi wa manispaa hiyo Mwalimu Mashelo Bahame ambapo amefafanua kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazosababisha watoto kukosa elimu lakini Serikali kwa kutambua hilo imeweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu japo jamii wakati mwengine inazidharau na kuzikejeli juhudi hizo.

'.. Zamani kulikuwa na makundi matatu yanayosimamia elimu kwa watoto wetu, jamii, walezi wakiwemo walimu na wazazi, Lakini siku hizi jamii imejitenga na jukumu hili na kundi la wazazi limejitenga pia wako na mambo mengine, Watoto wanalelewa na wafanyakazi wa ndani na luninga na haya mambo ya elimu wanayabeza hayana umuhimu kwao ..' Alisema 

Aidha Mwalimu Mashelo amelipongeza shirika la SOS kwa utekelezaji wa miradi ya elimu pamoja na kuwalea watoto waishio katika mazingira magumu ndani ya manispaa yake na mkoa wa Mwanza kiujumla huku akiwashukuru viongozi wa wilaya ya Ilemela Mkurugenzi Bi Ummy Mohamed Wayayu, Mbunge Dkt Angeline Mabula na kiongozi mkuu wa wilaya hiyo Mwalimu Hasan Elias Masala kwa juhudi zao katika kuunga mkono juhudi za kuboresha sekta ya elimu .

Kwa upande wake afisa elimu watu wazima manispaa ya Ilemela Mwalimu Recipius Masatu Magembe amesema kuwa mpango wa kutoa elimu kwa walioikosa  MEMKWA ulianza mwaka 1999 hadi 2022 kwa majaribio katika wilaya  za Kisarawe, Songea vijijini, Masasi, Musoma vijijini na Ngara na baada ya mpango kuonekana unafaa mwaka 2003 Serikali ikauingiza mpango huo katika shule zote nchini ili kuwasaidia watoto wote waliokosa elimu na Kwa wilaya ya Ilemela mpaka sasa zaidi ya watoto 1060 wamesajiliwa na wamekuwa wakifanya vizuri sanjari na kukemea dhana potofu ya kuamini elimu za nje ya darasa au kujiendeleza hazina manufaa yeyote .

Celestine Mwalongo ni mratibu wa miradi ya elimu katika shirika la SOS ambapo ameishukuru manispaa ya Ilemela kwa ushirikiano wake katika kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu inayofanywa na shirika lake huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya elimu .

Nae Mwalimu Sara Loom kutoka kabangaja shule ya msingi na Beatrice Magesa kutoka Kahama shule ya msingi kwa pamoja wameshukuru uwepo wa mafunzo hayo kwani yamewaongezea ubunifu katika kuwasaidia watoto wa awali na wanaoupata elimu nje ya mfumo wa kawaida.

Mafunzo kwa walimu na waratibu wa elimu kata yamefanyika kwa siku mbili kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la SOS ambapo lengo kuu ni kuwaongezea maarifa na ujuzi walimu kuweza kusimamia vizuri elimu katika maeneo yao.











Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • "TUUFANYE USAFI KUWA NI TABIA YA KUDUMUA": ANNA MBAO

    May 31, 2025
  • WATAALAM WA MANISPAA YA ILEMELA WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA MFUMO WA MANUNUZI WA UMMA

    May 29, 2025
  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.