Jamii imetakiwa kutunza na kulinda Ziwa Viktoria na mazingira yake ili liweze kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na cha baadae
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya halmashauri zinazozunguka Ziwa Viktoria LAVRAC ambae pia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Musoma Mhe William Gumbo ambapo ameupongeza uongozi wa ushirika wa wavuvi maarufu BMU wa kata ya Bugogwa unaosimamia mwalo wa Igombe kwa juhudi zao katika kuhakikisha mwalo huo unakuwa safi pamoja na kusisitiza kuwa ziara iliyofanywa na ushirika huo wa mamlaka za Serikali za mitaa ni sehemu ya uhamasishaji juu ya umuhimu wa kutunza Ziwa hilo na kulilinda
“Niwapongeze kwa utunzaji wa mazingira kiukweli mwalo ni msafi sana, Lakini hili lisiishie leo tuendelee kutunza Ziwa na mazalia yake”, amesema
Aidha Mhe Gumbo ameishukuru benki ya NMB kwa ufadhili wa tukio hilo sanjari na kuomba wadau wengine kuendelea kuunga mkono Serikali katika kulinda na kutunza mazingira
Kwa upande wake mwakilishi wa Mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni diwani wa kata ya Mecco Mhe Godlisten Kisanga mbali na kuwapongeza wananchi kwa ushirikiano wao katika zoezi la usafi amewaalika viongozi na wanachama wa jumuiya ya LVRAC kuwekeza wilaya ya Ilemela kwani wilaya hiyo ina maeneo mengi na fursa lukuki za kiuchumi
Nae meneja mwandamizi mahusiano na biashara za Serikali kutoka benki ya NMB Bwana Adelard Mang'ombe amesema kuwa benki yake mbali na utaratibu wa kawaida wa kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwenda kwa wananchi maarufu CSR, Benki yake imeongeza bilioni 2 katika bajeti yake kwaajili ya usafi na mazingira hivyo tukio lililofanyika leo ni sehemu ya kampeni wanazoziunga mkono juu mazingira
Nyabugumba Jonathan ni afisa mazingira wa manispaa ya Ilemela, Yeye amewasisitiza wananchi waliojitokeza katika tukio hilo kulifanya zoezi la usafi kama sehemu ya utamaduni wao na sio kusubiria kuhimizwa
Manispaa ya Ilemela imekuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa jumuiya ya halmashauri zinazozunguka Ziwa Viktoria kwa mwaka wa 2023 ambapo shughuli za kufanya usafi katika mwalo wa Igombe na upandaji miti katika kituo cha afya Karume zimefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli zilizopangwa kufanyika na jumuiya hiyo kabla ya mkutano wake mkuu wa mwaka utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Rock City Mall Ilemela jijini Mwanza na kuhudhuriwa na halmashauri zote wanachama wa nchi za Kenya, Uganda na Tanzania mwenyeji
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.