• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Maadili ya Msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • Utumishi na Utawala
        • Mipango na ufuatiliaji
        • Kilimo, Ufugaji na Uvuvi
        • Maendeleo ya Jamii
        • Elimu Sekondari
        • Elimu ya Awali na Msingi
        • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
        • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
        • Miundombinu na Uendelezaji wa Miji na Vijiji
      • Vitengo
        • Mazingira na Usafishaji
        • Maliasili na Uhifadhi Mazingira
        • Michezo, Utamaduni na Sanaa
        • Fedha na Uhasibu
        • Sheria
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Manunuzi
        • TEHAMA na Takwimu
        • Mawasiliano Serikalini
    • Kata
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

JAMII YA ILEMELA YATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA

Posted on: March 11th, 2023

Jamii ya Ilemela imetakiwa kutunza mazingira pamoja na kuwa na utamaduni wa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujiepusha na magonjwa ya milipuko


Rai hiyo imetolewa na afisa mazingira wa manispaa ya Ilemela Bi Jonathan Nyabugumba wakati wa zoezi la kufanya usafi na utoaji wa elimu juu ya kutunza mazingira na urejeshaji wa taka ngumu katika mialo ya manispaa ya Ilemela ambapo amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha maeneo yao wanayoishi pamoja na kutunza mazingira yanayowazunguka ili kujikinga na magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu kama vile kipindupindu na magonjwa ya tumbo


‘.. Tusipotunza mazingira yetu tutapatwa na magonjwa ya milipuko, Na huu ni wajibu wetu sisi wananchi sio mpaka Serikali itusimamie wapo mawakala katika maeneo yetu lakini na sisi tuna wajibu wa kufanya katika utunzaji wa mazingira ..’ Alisema

Aidha Bi Nyabugumba mbali na kuwashukuru wadau wa mazingira kutoka taasisi za chuo kikuu cha Dar es salaam, Arena recycling na Emedo ya jijini Mwanza amewataka wananchi kuendelea na utamaduni wa kufanya usafi hata baada ya taasisi hizo zinazotoa elimu ya mazingira kumaliza muda wao wa kazi ndani ya Ilemela pamoja na kusisitiza mawakala wa usafi kutekeleza wajibu wao katika maeneo yao ya kazi


Bahati Mayoma ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam shule ya sayansi akua na teknolojia ya uvuvi, yeye amewataka wananchi kutunza mazingira ya fukwe za ziwa viktoria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hakuna uingizaji wa plastiki ndani ya ziwa hilo, utekelezaji wa shughuli za kibinadam kando ya vyanzo vya maji sanjari na kuziasa BMU kusimamia wajibu wake ikiwemo usafi wa ziwa na mazingira yake pamoja na kubainisha tafiti mbalimbali zinazoelezea juu ya namna ziwa viktoria na mazalia yake vinavyoathiriwa na uharibu wa mazingira

Khamis Masimba ni mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Mihama na January Lucas ni mwenyekiti wa BMU ya mwalo wa Igombe wote kwa pamoja wameshukuru kwa elimu iliyotolewa ya utunzaji wa mazingira na urejeshwaji wa taka ngumu huku wakiahidi kuwasimamia wananchi wenzao katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kulindwa


Elimu juu ya utunzaji wa mazingira na urejeshaji wa taka ngumu imetolewa na taasisi ya ARENA kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es salaam kwa wananchi na viongozi wa mialo ya Kirumba, Mihama, Igombe na Kayenze ndani ya manispaa ya Ilemela kwa lengo la kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mazingira na kuzuia magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na mazingira machafu.



Announcements

  • TANGAZO KWA UMMA KUKUMBUSHWA KULIPIA VIWANJA March 28, 2023
  • MATOKEO KIDATO CHA NNE 2022 SHULE ZA SERIKALI NA BINAFSI MANISPAA YA ILEMELA January 29, 2023
  • HATUA ZA KUFUATA KUKATA LESENI KUPITIA MFUMO WA TAUSI April 13, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA September 30, 2022
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • MIKATABA YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 1.49 YASAINIWA ILEMELA

    May 18, 2023
  • SERIKALI KUCHUKUA HATUA KUDHIBITI MMOMONYOKO WA MAADILI

    May 17, 2023
  • BILIONI 61.3 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO ILEMELA

    May 15, 2023
  • KAMATI YA LISHE ILEMELA YAHIMIZA UTOAJI ELIMU MASUALA YA LISHE NA UTOAJI CHAKULA MASHULENI

    May 04, 2023
  • Tazama zaidi

Video

TANGAZO LA MRADI WA UWEKEZAJI WA GREEN ROCKY CITY
More Videos

Quick Links

  • Kuhakiki Taarifa za Mpiga Kura
  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip
  • Maombi ya leseni ya biashara

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.