Jamii ya Ilemela imehamasishwa kupanda miti sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 200 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi nchini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ndugu Said Kitinga ambae ni Katibu Tawala amesema upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira ni jambo linalohusu maisha ya binadamu wote.
“Jambo hili linahusu maisha yetu kwa ujumla wake pamoja na kizazi kilichopo na kinachokuja,tusipoweka mazingira yetu vizuri bado tunahatarisha maisha yetu.”Amesema Kitinga
Nae mwakilishi kutoka wakala wa misitu Tanzania (TFS) Tito Mwasumbi amesema wanaunga mkono juhudi za Mhe. Rais sambamba na kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mhe.Mpango juu ya upandaji miti isiyopungua 1,500,000 kila mkoa nchi nzima.
“Nyumba hizi zilizopo hapa jirani na shule hii ya Buswelu zitanufaika na uwepo wa miti hii pindi upepo unapokuwa mkali kwa kuwa miti inapunguza kasi ya uharibifu wa mazingira sambamba na kuzalisha hewa nzuri na kuleta mazingira ya kuvutia ni wajibu wa jamii hii kuhakikisha miti yote inakuwa kwa viwango vinavyokubalika.”Amesema Mwasumbi.
Mariam Samson ni mwalimu wa mazingira shule ya msingi Buswelu yeye anatoa shukrani kwa ugeni huo huku akiitaka jamii za jirani ya maeneo ya shule kuunga mkono juhudi hizo kwa kulinda miti hiyo isiibiwe wala kuharibiwa na mifugo.
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Buswelu Justin Winfred amezitaja faida za miti ambazo ni uwepo wa hewa safi ya oksijeni,vivuli wakati wa jua,mazingira yenye mvuto,mazao ya miti kama matunda na mbao ni faida kwa watumiaji.
Mrisho Mabanzo maarufu kama “Mr Tree” ambae ni balozi wa mazingira ameihamasisha jamii kupanda miti na kutunza mazingira kupitia kauli mbiu isemayo “Tanzania Yangu, Mazingira Yangu Nayapenda Daima”
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.