“ Usafi ni afya na afya ni usafi .”
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi.Ummy Wayayu alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba lililopo kata ya Ilemela wakati wa zoezi la kuhamasisha jamii kuwa na mazoea ya kupenda kufanya usafi kwenye maeneo yao kwa vitendo.
Pamoja na zoezi la usafi wafanyabiashara hao walipata fursa ya kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa soko lao na kumuomba Mkurugenzi na uongozi wa Halmashauri kuona namna bora zaidi ya kuimarisha miundo mbinu kama vyoo na kulipanua soko hilo ili wafanyabiashara wengi wapate nafasi ndani ya soko.
“ Soko hili ni salama watu wengi wanatamani kufanya biashara hapa changamoto ni ufinyu wa eneo na uwezeshwaji wa mitaji. “ Mwenyekiti wa soko la Sabasaba Khasim Hasani Msangi
Aidha Mkurugenzi Ummy amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Halmashauri yake ipo na mpango wa maboresho ya masoko yote ya ndani ya manispaa kwa kuzingatia kuwa masoko ni miongoni mwa vyanzo vya kuingiza mapato ambayo husaidia kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Nae diwani wa kata ya Ilemela Mhe.Wilbard kilenzi amewataka wananchi hao kuwa watulivu kuhusu suala la mikopo ya 10% ya wanawake ,vijana na walemavu kwani halmashauri miongozo na utaratibu mzuri wa kuanza kutolewa kwa mikopo hiyo.
Akihitimisha mkutano huo Mkurugenzi amewataka wafanyabiashara hao ambao tayari wana mikopo ya Halmashauri kukamilisha marejesho ya mikopo yao ili kutoa fursa kwa wahitaji wengine kukopa na kufanya zoezi la kuopesha kuwa endelevu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.