Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Adv.Mariam Msengi ambae pia ni katibu tawala wa Wilaya hiyo amepongeza idara ya afya kupitia kitengo chake cha lishe kwa kuendelea kufanya vizuri utekelezaji wa maadhimisho ya siku ya afya ya lishe katika mtaa (SALIM) yanayofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu ambapo huduma za afya, lishe, usafi wa mwili na mazingira,ulinzi wa mtoto na malezi shirikishi hutolewa.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kitengo cha lishe wakati wa kikao cha tathmini ya Wilaya kujadili taarifa ya lishe kuanzia Januari hadi Machi 2023/2024 Afisa lishe wa Wilaya hiyo Bi.Pilli Khassim amesema jumla ya mitaa 171 inayounda Halmashauri ya manispaa ya Ilemela iliweza kufikiwa na kutekeza SALIM sawa na 100% ya utekelezaji kwa mitaa yote.
“ Tulipanga kuwafikia wazazi 7,000 wenye watoto wa umri wa 0 hadi miezi 59 mpaka mwisho wa zoezi jumla ya wazazi 9,476 walifikiwa sawa na 135% ya lengo na 158% kwa watoto wa miezi 6 hadi 59 waliopatiwa matone ya vitamin A,wao tulipanga kutoa matone kwa watoto 5,000 na idadi ya waliofikiwa ilikuwa 7,918.” Amesema Afisa lishe (W).
Sambamba na pongezi kwa kazi nzuri Adv.Msengi amewataka wazazi kuhamasika katika suala la uchangiaji wa chakula shuleni huku akifafanua umuhimu wa watoto kupata chakula wakiwa shuleni.
“ Natamani na sisi Ilemela kiwango chetu cha elimu kiwe cha juu sana,ni muhimu wazazi na walezi kufahamu umuhimu wa watoto wetu kupata chakula wakiwa shuleni,tutapunguza utoro,tutaongeza usikivu na afya za watoto zitaboreka na kumpa mtoto fursa ya kufanya vizuri zaidi kitaaluma.”
Nae Mkuu wa polisi Wilaya ya Ilemela SSP.Egnatus B.Kapira amesema ni lazima vyanzo vya kukwamisha shughuli za lishe ndani ya Manispaa vifahamike ili nguvu iongezwe kwenye maeneo husika.
“Chakula kutolewa shuleni ni muhimu,hakuna sababu ya msingi ya kukwama kwa jambo hili kama ni elimu tuongeze kasi ya utaoaji elimu maeneo yote hasa yale yanayoonekana yapo nyuma zaidi.”
Akihitimisha kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Bi.Neema Semwaiko amesema ipo miongozo inayoendelea kutekelezwa kwa sasa, kuhusu masuala ya utoaji chakula shuleni sambamba na juhudi kubwa zinazoendelea kutekelezwa na uongozi wa Manispaa katika kuhakikisha shule zote ndani ya Manispaa zinatoa chakula
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.