Viongozi na watendaji wa Manispaa ya Ilemela wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya takwimu ili kufanya maamuzi kwa utashi wa kitakwimu kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika zoezi la sensa
Rai hiyo imetolewa na Ndugu Omary Mdoka, mkufunzi wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi na watendaji wa halmashauri ya manispaa ya ilemela
“Takwimu hizi ziwe chachu ziwe muongozo katika kutekeleza miradi mbalimbali kupanga mipango sambamba na utungaji wa sera”, alisema ndugu omary
Nae Ndugu Benedict Charles Mugambi, ambae ni meneja idara ya shughuli za kitakwimu Na Mkuu Wa Sehemu Ya Gis kutoka ofisi ya taifa ya takwimu akimwakilisha Mtakwimu Mkuu Wa Serikali amesisitiza juu ya matumizi ya matokeo ya senda katika masuala yote yanayopangwa kutekelezwa kupitia muongozo wa matumizi ya matokeo ya sensa uliotolewa na mhe rais
“Kazi yetu sisi ni kuwaonyesha namna ambavyo mnaweza kutafsiri matokeo ya sensa na ambavyo mtayatumia katika mipango mbalimbali”, alisema ndugu benedict
Matokeo ya sensa ambayo yametolewa hadi sasa na yamezinduliwa yamefanyiwa uchambuzi hadi ngazi ya kata /shehia lengo kikiwa ni kufika katika ngazi za mitaa na vitongoji hii ni miongoni mwa jambo linaloifanya sensa ya watu na makazi kuwa ya kipekee,
Akifungua mafunzo hayo Mhe Hassan Masala, Mkuu Wa Wilaya Ya Ilemela alisema kuwa Ilemela imejipanga kuhakikisha mipango na programu zote za maendeleo zinapangwa kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu na makazi, sensa ya majengo na sensa ya anwani za makazi ya mwaka 2022.
Wakichangia katika mafunzo hayo wenyeviti wa mitaa ya manispaa ya ilemela katika nyakati tofauti wameomba matokeo haya ya sensa yakatumike katika kupatikana ramani sahihi za maeneo yao ili ziweze kusaidia katika matumizi mbalimbali
Mwakilishi wa kundi la walemavu ameomba serikali kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya kuangalia shule ambazo zina elimu jumuishi ili ziweze kusaidia watoto wenye ulemavu waweze kupatiwa vipaumbele katika kupata elimu iliyo bora ili ikawapunguzie makali ya ulemavu.
Sambamba na mafunzo hayo, ofisi ya Taifa Ya Takwimu, ilikabidhi ramani ya manispaa ya Ilemela ikionyesha idadi ya watu kwa kata, pamoja na ramani za kwenye kata zikionyesha mgawanyiko wa watu na idadi yao kwa kila kata.
Kwa mujibu wa matokeo ya sensa, halmashauri ya wilaya ya ilemela ina idadi ya watu 509,687 kutoka watu 343,001 mwaka 2012. Kati ya idadi hiyo, watu 241,137 ni wanaume na watu 268,550 ni wanawake. Aidha, idadi hiyo inaonesha kiwango cha kasi ya ukuaji wa idadi ya watu katika manispaa yetu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita yaani kutoka mwaka 2012 hadi 2022 ni wastani wa asilimia 32
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.