Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela chini ya Mstahiki Meya Mhe. Renatus Mulunga, na Mkurugenzi Adv. Kiomoni Kibamba wamesaini mkataba wa ujenzi wa Barabara yenye urefu wa Kilomita 12.8 ambayo itajengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 23.48 fedha za kitanzania.
Barabara zitakazojengwa ni za Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongolo kwa urefu wa Km 9.5 na Barabara ya Buswelu-Busenga-Cocacola itajengwa kwa urefu wa Km 3.3
Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika tarehe 23/09/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa (Mb)
Mhe. Mchengerwa amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha miradi inasimamiwa vizuri ili kuhakikisha mikataba inatekelezwa kwa wakati na viwango vya juu.
Sambamba na hilo Mhe Mchengerwa amewataka wakandarasi kuhakikisha wanaingia site mara moja na kukamilisha kazi kwa muda uliopangwa.
Utekelezaji wa ujenzi wa Barabara hizi utafanyika ndani ya kipindi cha miezi 15, chini ya mkandarasi Nyanza Road Works ambapo mkandarasi mshauri M/s NIMETA Consult (T) Ltd ndie atakaesimamia kazi hiyo kwa muda wa miezi 28 kwa maana miezi 16 ya kuwa site na miezi 12 ya matazamio.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.