Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Eng. Modest Apolinary na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa Bi Celine Robert wamesaini mkataba wa makubaliano wa uanzishaji wa mradi wa uboreshaji wa mifumo ya usafiri mijini.
Mradi huu ambao unatarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu mwishoni mwa Mwaka 2023 unatarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Jiji la Mwanza
Mradi huu utafadhiliwa na shirika la maendeleo Ufaransa(AFD) ambayo ni sehemu ya miradi inayotekelezwa katika programu ya "GREEN AND SMART CITY SASA"
Akishuhudia utiaji wa saini,ndugu John Cheyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambae alimwakilisha Katibu Mkuu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa ya Ilemela na jiji la Mwanza kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa mtaalam mshauri wa mradi huu.
"Niwatake wakurugenzi kuhakikisha mnatoa ushirikiano wa kutosha pamoja na kuhakikisha mradi utakapokuwa unaanza rasmi mnachagua wataalam sahihi ili mradi ukamilike kwa usahihi na kwa wakati uliokusudiwa"amesema John Cheyo.
Bi Celine Robert ambae ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) ameshukuru kwa hatua iliyofikiwa na kusema kuwa lengo hasa la mradi huu ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupunguza matumizi ya hewa ukaa kwa kuboresha usafiri mjini
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.